Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) imewataka wakenya kuwa macho, ili kujiepusha na matapeli wanaohadaa watu kwa kuwapa vyeti ghushi vya kuidhinisha uadilifu wao almaarufu Clearance Certificate.

Katika chapisho kwenye mitandano yao EACC imesema Watapeli hao wamekuwa wakiwalipisha watu kiasi fulani cha fedha kwa ahadi ya kuwapatia vyeti hivyo vya kuidhinisha uadilifu.

Aidha, walaghai hao pia wamekuwa wakituma notisi kwa mashirika mbalimbali, wakiwataka kufanya uchunguzi fulani. Tume hiyo imebainisha kuwa huduma zao hazihusishi malipo yoyote, na hivyo kuwaomba Wakenya kutoa taarifa zozote wanazozijua kuhusu shughuli hizi za udanganyifu.

Share the love
July 18, 2023