Mabalozi na Makamishna Wakuu nchini Kenya wameelezea wasiwasi wao kuhusu ghasia na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya hivi majuzi dhidi ya serikali yaliyoitishwa na upinzani.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumanne, wajumbe wa nchi 13 zikiwemo Australia, Canada, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswizi, Ukraine, Uingereza na Marekani, zimetoa wito wa kufanyika mazungumzo kati ya Rais William Ruto na upinzani unaoongozwa na Raila Odinga ili kutatua tofauti zao kwa amani.

Wajumbe hao walionyesha utayarifu wa kupatanisha serikali na upinzani, wakisema, wako tayari kuunga mkono vyama katika juhudi zao za kutafuta suluhisho la kujenga na la amani.

Share the love
July 18, 2023