Naibu Inspekta Jenerali (DIG) wa Polisi Eliud Kipkoech Lagat amejiondoa ofisini kwa muda ili kupisha uchunguzi kuhusu mauaji ya Albert Ojwang’.

    Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari na taifa kwa ujumla, Lagat amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na asasi zinazofanya uchunguzi katika kutoa taarifa muhimu itakayohitajika.

    Vilevile ameongeza kuwa amekabidhi majukumu yake kwa naibu wake. Hatua ya Lagat inajiri baada ya shinikizo kutoka kwa wakenya ambapo baadhi ya wakenya waliandamana Jumanne iliyopita wakitaka Lagat ajiuzulu huku uchunguzi ukiendelea.

    Hata hivyo aliyekuwa jaji Mkuu David Maraga amesema kuwa kujiondoa kwa Lagat kutoka kwa wadhifa wake ni hatua ya kwanza na sasa anatakiwa kujiuzulu, kukamatwa na kushtakiwa.

    June 16, 2025

    Leave a Comment