BY ISAYA BURUGU 30TH DEC 2022-Gavana wa  kaunti ya Meru Kawira mwangaza ameponea kungatuliwa afisini baada ya bunge la seneti kusema kuwa madai ya ukiukaji sheria yaliyotolewa dhidi yake hayana msingi wowote.

Katika  Kikao hicho kilitishwa na spika wa seneti Jeffa Kingi kutathmini ripoti ya kamati ya bunge hilo iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza msingi ambao ulipelekea wawakilishi wadi wa kaunti ya meru kupiga kura ya kumng’atua afisini gavana huyo,mwenyekiti wa kamati hiyo Bonny Khalwale amesem akuwa baada ya tathmini ya kina kuhusu madai yaliyotolewa na wawakilishi wadi wa Meru dhidi ya gavana wao,wamegundua kuwa hayana msingi.

Mwangaza alikuwa anakumbwa na mashataka manne tofuati ya ukiukaji sheria yote ambayo yamepuziliwa mbali na kamati hiyo.

Kufuatia hayo spika wa seneti Jeffa Kingi ametangaza kuwa majadala wowote kuhusu swala hilo unafikia kikomo kama inavyohitaji sheria.

Hatua hiyo sasa inamanisha kuwa Kawira ataendelea kuhudumu kama gavana wa Meru.

 

 

December 30, 2022