BY ISAYA BURUGU  30TH DEC 2022-Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen ameamuru kusimamishwa kwa leseni ya uendeshaji wa Mabasi ya Modern Coast mara moja.

Katika taarifa iliyoandikwa Ijumaa, Desemba 30, CS Murkomen alibainisha kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA).

“Kufuatia ajali ya tarehe 28 Desemba, nimeagiza NTSA isitishe shughuli zote za kampuni ya basi ya Modern Coast mara moja, huku uchunguzi kuhusu ajali hiyo ukiendelea,” akasema.

Murkomen alifafanua kuwa leseni hiyo ilifanywa upya mnamo Novemba baada ya kampuni hiyo ya mabasi kutii kanuni zilizowekwa na NTSA.

“Shughuli hizo ziliruhusiwa kuanza tena Novemba mwaka huu baada ya kampuni hiyo kufuata masharti yote ambayo walikuwa wamejiwekea.

December 30, 2022