Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amewaagiza maafisa kutoka idara ya kukabiliana na majanga nchini, kuimarisha jitihada zake za kuwasaidia wananchi mjini Narok wakati wanapokumbwa na majanga ya moto.

Akizungumza baada ya kuzuru maeneo 5 yaliyoathirika na moto mjini Narok, gavana Ntutu ameahidi kuongeza idadi ya magari ya kuzima moto ili kuhakikisha kuwa ajali za aina hii zinakabiliwa haraka iwezekanavyo punde zinapotokea.

Gavana Ntutu aliyeandamana na mwakilishiwadi wa Narok mjini Lucas Kudate pamoja viongozi wengine wa serikali ya kaunti alisikitikia matukio haya, akisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha ajali hizi.

Katika kipindi cha mwezi mooja ajali za moto zimeshuhudiwa katika eneo la Total, Mong’are, KAG, eneo la Kwa Muchai, na Double M.


YouTube player

January 12, 2023