BY ISAYA BURUGU  13TH JAN 2023-Rais  William Ruto  Hivi leo Ijumaa anaazna  ziara ya siku mbili eneo la Nyanza .Ziara hiyo ya Rais  itampelekea kuzuru kaunti tatu za Nyanza ambazo ni Homa Bay,Kisumu na Siaya.

Kwa mjibu wa msemaji wa Ikulu Hussein Muhamed , ziara hiyo inajumuisha kuzindua  na kukagua miradi ya nyumba katika eneo hilo ikiwemo kuanzisha  matumizi ya soko jipya la manispaa ya Homa Bay  lililomalizika hivi maajuzi   sawa  na kukutana na viongozi  eneo hilo Pamoja na wenyeji.

Ziara hiyo inaanzia Homa bay ambapo rais Ruto atazindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 5000 za makaazi kwa gharama nafuu katika kaunti hiyo.

Muhamed akizungumza na wandishi Habari jana aidha alifafanua mafanikio yaliyoafikiwa katika utekelezaji wa agenda ya makaazi tangu rais Ruto kuchukua hatamu akidokea kuwa serikali inalenga kujenga nyumba 200,000 kila mwaka.

 

 

 

 

 

January 13, 2023