Naibu Gavana Mteule wa Kisii Elijah Obebo

Gavana wa Kaunti ya Kisii Simba Arati amemteua Elijah Obebo kuwa naibu wake mpya, baada ya kubanduliwa kwa aliyekuwa naibu gavana, Robert Monda.

Uteuzi huu umetangazwa kwa bunge la kaunti ya Kisii na Spika Philip Nyanumba katika vikao vya Jumatano. Spika Nyanumba amewasilisha jina la Obebo kwa Bunge la Kaunti hiyo ili kuwapa wawakilishiwadi nafasi ya kujadili pendekezo hilo na kisha kumuidhinisha au kupinga uteuzi huo.

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Obebo amekuwa akihudumu kama Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi wa Umma.

March 20, 2024