BY ISAYA BURUGU 4TH SEPT,2023-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amemsuta kinara wa azimio la umoja Raila Odinga kwa matamshi yake alipozuru kaunti ya Narok  jana.

Ntutu akizungumza alipongoza uzinduzi wa  eneo pana la kiviwanda kule  la Limanet viungani mwa mji wa Narok, aliyataja matamshi hayo ya Odinga kama ya chki.Antony Mintila ana mengi Zaidi.Amesema Odinga alitoa  matamshi ya chuki hatua ambayo amesema huenda ikalemaza  ushirikiano kati ya  viogozi kaunti ya Narok na kumtaka kiogozi huyo kuheshimu viogozi wengine..

Kwa upande wake kamishana wa kaunti ya Narok Isaac Masinde amewataka wanaopinga miradi ya serikali kukoma kuingilia mipango ya serikali kuanzisha viwanda mjini Narok.

Naye mbunge wa Narok kaskazini Agness Pareyio amesifia kazi ya gavana Ntutu eneo la Limanet baada ya miradi ya maji kuzinduliwa akisema hatua hiyo imepelekea eneo hilo kuwa safi kibiashara.

 

 

Share the love
September 4, 2023