BY ISAYA BURUGU,12TH DEC 2023-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amehaidi kushirikiana na vikosi vya usalama kuwakamata wahalifu mjini Narok.

Ntutu akizungumza katika madhimisho ya siku ya Jamhuri katika shule ya msingi ya Suswa Narok mashariki ameshutumu hatua ya wahalifu kuwavamia wakazi wa mji wa Narok na kuunga mkono hatua ya kutangazwa hali ya dharura mjini Narok hatua inayolenga kukabili ongezeko la uhalifu.

Gavana huyo aidha  amewapongeza maafisa wa  usalama kwa oparesheni ambayo imepelekea kunaswa kwa wahalifu 141 usiku wa kuamkia leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

December 12, 2023