BY ISAYA BURUGU,12TH DEC,2023-Rais William Ruto amethibitisha kumvika mwanariadha mshikilizi mara mbili wa rekodi za dunia Faith Kipyegon kwa tuzo ya juu Zaidi ya Elder of the Order of the Golden Heart of Kenya (E.G.H.)Kuvikwa huku kunajiri saa chache tu baada ya Kipyegon kushinda tuzo ya mwanariadha bora wa kike kote duniani katika hafla iliyofanyika usiku wa leo ya bodi ya riadha duniani.

Rais Ruto alithibitisha hili wakati wa hotuba yake ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Kenya, sikukuu ya Jamhuri katika uwanja wa Uhuru Gardens jijini Nairobi, hivi leo.

Kiongozi huyo wa taifa pia alimsifia Kipyegon akisema kwamab safari yake ya mafanikio ni kichocheo safi kwa wanariadha chipukizi lakini pia akawapongeza wanariadha wengine ambao wamekuwa wakiipeperusha bendera ya Kenya katika michezo mbalimbali mwaka huu

.

Order of the Golden Heart of Kenya ndio kitengo cha juu zaidi cha tuzo za urais ambacho kimegawanywa zaidi katika madaraja matatu: Chief of the Order of the Golden Heart of Kenya (C.G.H.), Elder of the Order of the Golden Heart of Kenya (E.G.H.) na Moran of the Order of the Golden Heart of Kenya (M.G.H.)

December 12, 2023