Gavana wa kaunti ya Nyamira Amos Kimwomi Nyaribo ameondolewa madarakani. Wawakilishi wadi 23 kati ya thelathini na moja waliohudhuria kikao hicho walipiga kura kuunga mkono hoja hiyo.

    Wengine wanne walikuwa wamemwandikia Spika wakiomba kujumuishwa katika upigaji kura.Hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni na mwakilishi Wadi wa Bonyamatuta Julius Kimwomi Matwere, ilitaja madai ya matumizi mabaya ya ofisi na ukiukwaji wa taratibu za kisheria.

    Gavana Nyaribo alishtakiwa kwa kuendesha shughuli za kaunti kupitia vikao visivyoidhinishwa vya “Bunge Mashinani”, ambavyo havikutambuliwa kisheria.

    Vilevile Hoja hiyo ilimkashifu zaidi kwa kuidhinisha na kutumia bajeti ya kaunti kuidhinisha Peris Nyaboke-Oroko kama Waziri wa Kilimo wa Kaunti, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mzozo katika bunge la kaunti hiyo.

    November 25, 2025

    Leave a Comment