Kiongozi wa chama cha Republican Kevin McCarthy amechaguliwa kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani katika jaribio la kihistoria la 15, baada ya siku kadhaa za duru za upigaji kura kushindwa kufanikiwa.

Warepublican walishangilia wakati ushindi wake ulipotangazwa huku wakiimba. McCarthy akiwa na hamu ya kukabiliana na rais wa Marekani Joe Biden na Wanademokrats akisema kazi sasa inaanza.

Baada ya kuchaguliwa, McCarthy alikula kiapo cha ofisi, na hatimaye bunge liliweza kuwaapisha wabunge wapya waliochaguliwa ambao walikuwa wakisubiri kwa wiki nzima bunge kufunguliwa rasmi na kikao cha 2023-24 kuanza.

January 7, 2023