Siku kadhaa baada ya mgao wa fedha za maendeleo ya maeneobunge almaarufu NG CDF kutolewa, mbunge wa Thika Mjini Alice Ng’ang’a ameaka kuongezwa kwa fedha hizo hasa katika maeneobunge yaliyo na idadi kubwa Zaidi ya watu.
Bi. Ng’ang’a amesema kuwa kupatiwa fedha sawa na maeneobunge yaliyo na idadi ndogo ya wananchi kutarudisha nyuma kiwango cha maendeleo yanayotekelezwa chini ya mipango ya fedha hizo.
Hazina ya kitaifa ilikubali kutoa mgao wa fedha hizi kwa maeneobunge huku uamuzi kuhusu uhalali wa mgao huu ukiendelea kusubiriwa, nao wabunge wakitafuta mbinu za kuhakikisha kuwa fedha hizi zitaanza kutolewa kwa njia iliyojikita katika sheria.