NAROK,1ST FEB,2023-Hatimaye stendi mpya ya magari imefunguliwa mjini Narok. Hafla ya ufunguzi wa stendi hiyo imeongozwa na waziri wa ardhi katika serikali kuu Zacharia Njeru na gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu.

Gavana Ntutu amesema kuwa ujenzi wa stendi hiyo umefanikishwa  kupitia juhudi za serikali ya kaunti ya Narok,ile yakitaiafa na benki ya Dunia.

Stendi hiyo mpya ambayo imekuwa ikijengwa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja uliyopita ina jumla ya maeneo 116 ya kupakia magari ,afisi tano  na   vyumba vitatu.

Picha:Radio Osotua
Akizungumza katika hafla hiyo waziri wa ardhi Zacharia Njeru  amesema wakati umewadia kwa wenyeji wa kaunti ya kukumbatia maendeleo kutoka kwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Narok.
Njeru amesema serikali imeweka mipango ya kuboresha mji wa Narok na miji mbali mbali nchini. Aidha  ameongeza kuwa  serikali inapanga mikakati ya  ya kuwapa vyeti vya kumiliki ardhi wakazi wa Narok.
Kauli yake imeungwa mkono na gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu akisema wamiliki wa magari wana hadi siku nane ili kuanza kutumia rasmi kituo hicho. Ntutu amesema serikali yake inapania kuleta mabadiliko katika mji wa Narok yanayojumuisha  kuinua hadhi ya mji wa Narok.
February 1, 2023