BY ISAYA BURUGU 1ST FEB,2023-Wakaazi wa eneo la London viungani mwa mji wa Narok wanakadiria hasara baada ya moto kutokea katika nyumba yao ya makaazi. Moto huo uliozuka leo asubuhi umeteketeza nyumba moja kati ya kadhaa zinazopaka nayo.Brigid Agwenge anaripoti kwa kina.

 Kwa mujibu wa walioshuhudia,chanzo cha moto huo ulioteketeza nyumba moja kati ya nyumba kadhaa bado hakijabainika kikamilifu ila wanadai kuwa huenda ulisababishwa na hitilafu ya umeme. Aidha wakaazi hao wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuwasilisha magari ya kuzima moto sawa na vifaa ili kukabili majanga ya moto yanapoibuka.

Ni majuma matatu tu tangu mkasa wa moto uliposhuhudiwa katika eneo la mong’are na kuwaacha wakaazi wa eneo hilo bila makaazi.

 

 

 

 

February 1, 2023