BY ISAYA BURUGU,5TH DEC 2023-Hazina ya husler imeweza kutoa mkopo wa kima cha shilingi bilioni 41 kwa zaidi ya wakenya milioni 22 tangu kuanzishwa kwake kwa mjibu wa takiwmu za hivi punde kutoka kwa serikali.

Hazina hiyo ambayo imepokea shutuma na sifa kwa usawa,imeshuhudia ongezeko la wakenya wanaomba mikopo kutoka kwa hazina yenyewe kutoka shilingi bilioni 39 hadi shilingi bilioni 41 katika kipindi cha juma moja lililopita.

Idara ya serikali ya biashara za kadri na zile ndogo ndogo,imetangaza mipango ya kuanzishwa kwa hazina ya MSME inayolenga wafanyibaishara wa kadri na wadogo wadogo.

Wizara imelezea kutamaushwa kwake ,na amshambulizi yanayoelekezewa wafanyibaishara wadogo na maafisa wa serikali ya kaunti haswa Nairobi,ikiongeza kuwa serikali kwa sasa imo mbiyoni kuanzisha hazina ya wafanyibaishara wadogo inayolenga sekta isiyokuwa rasmi.

 

December 5, 2023