BY ISAYA BURUGU,5TH DEC 2023-Kizazaa kimeshuhudiwa leo  Bungeni wakati wabunge walipoandaa matembezi kuhusu kushindwa kwa Serikali kutoa pesa zilizokusudiwa kwa Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF).

Wabunge hao ambao wanatarajiwa kuendelea na mapumziko siku ya Alhamisi, walimaliza kikao cha Baraza kabla ya wakati wake na kuanza kuimba nyimbo.

Sehemu ya wabunge hao ilizuia hata mlango wa Bunge na kuwazuia wenzao kuingia ndani ya Bunge hilo, huku Kinara wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Sylvanus Osoro akiwa mmoja wa wale waliotolewa kwa nguvu.

.Hii si mara ya kwanza kwa wabunge kufanya mvutano na serikali kuhusu fedha za CDF; Februari mwaka huu, walitishia kutatiza upitishaji wa bajeti ya nyongeza iwapo fedha hizo hazitatolewa kwa wakati.Haya yalijiri baada ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa bodi ya NG-CDF Yusuf Mbuno kuwaambia wabunge kwamba ni Ksh.10 bilioni pekee kati ya Ksh.44.2 bilioni zilizokusudiwa kutolewa ndizo zimetolewa.

 

December 5, 2023