BY ISAYA BURUGU,30TH AUG 2023-Waziri wa Africa mashariki na maeneo kame nchini Rebbecca Miano amesema baa la njaa limepungua humu nchini kutoka  zaidi watu milioni 4.4 hadi watu milioni mbili 2.8 mwaka huu.

Akizungumza alipozuru Kampuni ya mamlaka ya Maendeleo Ewasonyongiro kusini Mjini Narok, waziri Miano amesema hatua hiyo imeafikiwa kutokana na juhudi za  serikali yakitaiafa kutoa mbolea ya bei nafuu  hali  ambayo imepelekea wakulima kuvuna mazao yao kwa njia bora mwaka huu.

Aidha Waziri huyo amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 33 kufanikisha juhudi za maeneo kame kupata chakula hatua ambayo amesema itachagia wakaazi wa maeneo hayo haswa  watoto wachanga kupata chakula cha kutosha .

 

 

August 30, 2023