BY ISAYA BURUGU,25TH MARCH,2023-Idara ya usalama kaunti ya Mombasa imewahakikishia waumini wa dini ya kislam kuwa usalama wao utaimarishwa vya kutosha wakati huu wa msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo idara hiyo imewataka wakaazi kushirikiana kikamilifu na maafisa wa polisi ili kukabili yeyote aliye na nia ya kufuruga amani.Kaimu kamishna wa Mombasa Ronald Mwiwawi,amesema kuwa idara ya usalama imeangazia swala la usalama wakati huu kwa makini.Amewaraia waislamu kuendelea na sala zao bila wasiwasi.

Mwiwawi aliyezungumza baada ya kuongoza kikao cha usalama na viongozi mbali mbali kaunti ya Mombasa,amewataka wazazi kuajibikia malezi ya Watoto wao na kuwalinda dhidi ya kuingilia makundi ya uhalifu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

March 25, 2023