Rais William Ruto kwa mara nyingine ameendeleza shutuma zake dhidi ya viongozi wa upinzani, akiwataka kumkabili moja kwa moja badala ya kuhitilafiana na Maisha ya wakenya wa kawaida.

Akizungumza katika kaunti ya Kisii adhuhuri ya leo, rais amesema kwamba wakenya hawakumbwaga katika uchaguzi mkuu ila yeye ndiye aliyemshinda, hivyo basi anafaa kumenyana naye pasi na kuwahangaisha wakenya kwa maandamano.

Awali rais Ruto na viongozi wengine walihudhuria hafla ya shukrani kwa ajili ya Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu katika eneo la  Nyaribari Masaba, katika Kaunti hiyo ya Kisii. Gavana wa Kisii Simba Arati, alitoa wito kwa viongozi wote kuzika tofauti zao za kisiasa, na kuwafanyia wananchi kazi.

Wengine waliohudhuria ni Pamoja na Naibu rais Rigathi Gachagua na pia mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.

March 24, 2023