Mamlaka Huru ya Kutathmini utendakazi Polisi (IPOA) imetangaza kuwa faili kadhaa za uchunguzi zitatumwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), huku ikithibitisha kujitolea kwake kwa uwajibikaji na uwazi katika kushughulikia utovu wa nidhamu wa polisi.

    Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari, Mwenyekiti wa IPOA Ahmed Isaack Hassan alisema kuwa mamlaka hiyo haitatishwa inapotekeleza majukumu yake.

    Alifichua kuwa ni asilimia 25 tu ya malalamishi yaliyopokelewa yanatoka ndani ya huduma ya polisi, wakati idadi kubwa zaidi asilimia 75 ni kutoka kwa umma, na hivyo kusisitiza upungufu wa uaminifu kati ya raia na idara ya polisi.

     

    June 23, 2025