BY ISAYA BURUGU ,1ST NOV,2022-Jamaa za watu walipotea eneo la pwani sasa zinaitaka serikali kuingilia kati na kuwatafuta jamaa hao na kuwarudishia wakiwa hai au iwapo walifariki wapate kufahamishwa.

Wakizunguza na wandishi Habari jijini Mombasa jamaa hao wamelezea jinsi jamaa wao walipotoweka na kutokomea baada ya kudaiwa kukamatwa na watu waliojidai kuwa maafisa wa polisi.

Wanasema kuwa ni afueni kwao kwa serikali kutangaza vita dhidi ya mauaji ya kiholela na kutoweka kwa watu kwa njia tatanishi na sasa ni sharti juhudi zote ziwekwe kuwapata jamaa zao. Inadaiwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita Zaidi ya familia mia mbili hazifahamu walipo jamaa wao.

Mathews Jipeta  afisa kutoka shirika la haki za kibinadamu la Haki Afrika  amesema kuwa wana imani kuwa haki itatendeka.

 

 

 

 

November 1, 2022