BY ISAYA BURUGU,1ST NOV,2022-Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula ameunga mkono mapendekezo ya rais William Ruto ya kuwahoji mawaziri wa wizara mbalimbali bungeni.

Akizungumza wakati wa mahojiano ya kipekee katika radio mojawapo humu nchini, Wetangula amesema kuwa wako katika harakati ya kubadilisha utaratibu bungeni ambapo watatenga siku moja kila wiki ili kila waziri afike mbele ya wabunge na kujibu maswali.

Hali kadhalika ameeleza kuwa hatua hiyo itawafanya mawaziri kuwajibika Zaidi katika kutekeleza majukumu yao

November 1, 2022