Jeshi la Kongo limewashutumu waasi wa M23 kwa kuwaua takriban raia 50 katika mji wa mashariki wa Kishishe.

Haya yanajiri huku kukiwa na taarifa za mauaji ya watu wengi kufuatia kuanza tena kwa mapigano, huku usitishaji mapigano uliokubaliwa wiki iliyopita ukionekana kuporomoka. Kundi hilo la waasi limekanusha madai dhidi yao likisema kuwa halijawahi kuwalenga raia.

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilikubaliana katika mazungumzo nchini Angola kwamba usitishaji vita utaanza kutekelezwa Ijumaa iliyopita.

M23 walisema mapatano hayo hayakuwahusu kwani hawakualikwa kwenye mazungumzo hayo.

December 2, 2022