Isiolo Diocese

Waumini wa kanisa katoliki katika kaunti ya Isiolo na maeneo jirani wana kila sababu ya kutabasamu sasa, baada ya kupandishwa hadhi kwa Vikarieti ya Isioli hadi kuwa jimbo katoliki la Isiolo, katika hafla iliyoandaliwa kutwa ya leo.

Jimbo katoliki la Isiolo litaongozwa na Askofu Anthony Ireri Mukobo ambaye pia alisimikwa kama askofu wa kwanza wa jimbo hilo ambao lilikuwa vikarieti ya kichungaji tangu mwaka wa 1995, tangu ilipogawanywa kutoka kwa jimbo katoliki la Meru.

Hafla za leo ziliandaliwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Eusebius Isiolo ambalo litakua makao makuu ya Jimbo hilo.

April 22, 2023