Rais William Ruto amevunja kimya chake kuhusiana na matukio katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifu, ambapo miili Zaidi inaendelea kufukuliwa, ikihusishwa na wafuasi walioaga dunia baada ya kujinyima chakula na maji. Rais amelaani imani inayosambaza na Mshukiwa wa aliyetambuliwa kama Kasisi Makenzi, akieleza kwamba watu wanaoeneza Imani inayokiuka katiba nchini wanafaa kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika hafla ya kufuzu kwa mahafali 222 waliotoka katika chuo cha mafunzo ya mafias awa magereza eneo la Ruiru kaunti ya Kiambu mchana wa leo,rais aidha ametoa onyo kali kwamashirika yanayojihusisha na utoaji wa mafunzo ya kupotosha, akisema kuwa watu na mashirika kama haya yanapaswa kukabiliwa kama magaidi humu nchini.

Wakati hayo yakijiri ni kuwa Washukiwa 14 wametiwa nguvuni wakihusishwa na vifo vya halaiki katika msitu wa shakahola katika kaunti ya Kilifi. Haya ni kwa mujibu wa Inspekta jenerali wa polisi Japheth Koome, ambaye alizuru eneo hilo mchana wa leo. Akizungumza na waandishi wa habari muda mapema leo, Koome alidhibitisha kuwa miili 11 zaidi imefukuliwa katika eneo hilo, na kuifikisha idadi ya watu wote walioaga dunia kutokana na imani hii hadi 58.

Inspekta generali aidha ameeleza kwamba mshukiwa mkuu katika matukio yaliyosababisha vifo hivi Paul Makenzi ameshtakiwa na hata kufikishwa mahakamai hapo awali akihusishwa na mauji ya Watoto.

April 24, 2023