Kadinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, ataongoza Ibada ya Kufunga Jeneza la Hayati Papa Mtakatifu Francis, kabla ya mazishi ya papa Jumamosi asubuhi.
Ibada ya kiliturujia itahudhuriwa na Makardinali kadhaa na viongozi wa Jimbo kuu. Kufungwa kwa jeneza hilo, kutaashiria mwisho wa umma kuutazama mwili wa papa katika Basilica ya Mtakatifu Petro, ambayo imeshuhudia makumi ya maelfu ya watu wakitoa heshima zao kwa marehemu Papa.
Basilica ya St. Peter ilisalia wazi hadi 5:30 AM siku ya Alhamisi, ikifungwa kwa saa moja na nusu kabla ya kufunguliwa tena saa 7:00 AM kwa Waumini kuendelea kutoa heshima zao za mwisho.
Cardinal Kevin Farrell, Camerlengo of the Holy Roman Church, will preside at the Rite of Sealing of the Coffin of the late Pope Francis on Friday, April 25, at 8:00 PM, ahead of the papal funeral on Saturday morning.
The liturgical rite will be attended by several Cardinals and… pic.twitter.com/7jN1ROsL91
— Vatican News (@VaticanNews) April 24, 2025
Wakati hayo yakijiri, humu nchini viongozi mbalimbali wakiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula na kinara wa ODM Raila Odinga, hii leo walizuru ofisi ya mwakilishi wa papa nchini Kenya Askofu mkuu Bert Ven Megen kutoa heshima zao.
Wetangula aliendelea kusifu dhamira isiyoyumba ya Papa kwa ubinadamu, harakati zake za kutafuta amani bila kuchoka, utetezi kwa walio hatarini, na kutoa wito kwa viongozi wa kimataifa kujenga madaraja ya umoja badala ya kuta za migawanyiko.
Kwa upande wake bw. Odinga alikumbuka wito wa Papa wa kusitishwa kwa mapigano katika Mashariki ya Kati na juhudi zake za kudumu za kuleta unafuu kwa watu kote ulimwenguni.
This morning, joined by several Members of the National Assembly, we visited the Apostolic Nunciature in Nairobi to pay tribute following the passing of His Holiness, Pope Francis.
In honouring his remarkable life, I recognized the Pope’s unwavering commitment to humanity, his… pic.twitter.com/vzmXD4Nz07
— Rt.Hon.Dr.Moses Wetang’ula (@HonWetangula) April 24, 2025