Thika Level 5 Hospital

Hospitali za kiwango cha Level 5 kote nchini zinahitajika kuwa na mdaktari wengi waliofuzu pamoja na mashine za matibabu zinazohitajika ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa wepesi.

Kauli hii imetolewa na kamati ya bunge la seneti inayotathmini maswala ya afya, baada ya kuwahoji wahudumu wa Afya kutoka katika hospitali ya Thika Level 5 ambapo mtoto Travis Maina alifikishwa kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kutokana na ukosefu wa huduma zinazohitajika.

Mtoto huyo wa miaka 2 aliaga dunia baada ya kuuguza jeraha la kichwa kwa kudungwa kwa jembe la Uma, jambo ambalo linaendelea kuchunguzwa na kamati hiyo ya seneti. Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago, ameeleza kuwa huduma za afya zinafaa kupewa kipaumbele katika serikali za kaunti.

November 8, 2022