Tume ya Kitaifa ya Huduma Kwa Polisi imepata msemaji mpya.Dkt Resila Atieno Onyango sasa ndiye msemaji mpya wa tume hiyo.

Bi. Onyango ndiye Mwanamke wa pili kuhudumu kama msemaji  wa polisi nchini ambapo amechukua nafasi ya Bruno Shioso ambaye alipandishwa cheo na kuteuliwa kuwa kamanda wa Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Huduma ya Polisi huko Kiganjo.

Bi. Onyango anaingia ofisini wakati tume hiyo inakabiliwa na tatizo la taswira kutokana na madai ya mauaji ya kiholela na aina nyingine za unyanyasaji.

Aligonga vichwa vya habari mwaka jana alipokuwa afisa wa polisi wa kwanza wa kike, katika historia ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi, kupata digrii ya udaktari.Yeye ni Mratibu Mwandamizi wa Polisi na kwa sasa ni Naibu Mkurugenzi wa Mipango katika Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi.

November 8, 2022