BY ISAYA BURUGU,6TH SEPT,2023-Kamati kuu ya chama cha ODM imafikia kumtimua chamani mbunge wa Gem  Elisha Odhiambo , Seneta wa Kisumu Tom Ojienda  mbunge wa Bondo  Gideon Ochanda , mbunge wa Langata Felix Odiwuor  na Caroli Omondi  ambaye ni mbunge wa eneo bunge la Suba kusini.Viongozi hao wametimuliwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama.

Aidha ODM kimemtoza faini Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passaris kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama na kupigia kura Mswada wa Fedha wa 2023, ambao sasa ni Sheria.

Katika taarifa yake hivi leo, chama hicho kilisema Passaris atalazimika kulipa Sh250,000 kama faini kwa kukaidi chama kando na kuomba msamaha kwa maandishi ndani ya siku saba.Chama hicho kimesema azimio hilo lilifikiwa wakati wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama hicho iliyofanyika leo  chini ya uongozi wa kiongozi wa Chama Raila Odinga.

Chama hicho kimesema NEC iliitishwa baada ya mfululizo wa vikao vilivyofanywa na vyombo vingine vya chama vikiwemo Kamati Kuu ya chama, Kamati ya Nidhamu na Bodi ya Taifa ya Uchaguzi.

Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Kitaifa John Mbadi.

Passaris alikuwa miongoni mwa wanachama 28 wa Orange Democratic Movement ambao walikaidi chama na kuupigia kura Mswada huo mnamo Juni 14.Chama hicho kilisema pia kitawaadhibu wabunge ambao hawakuwapo wakati wa zoezi la upigaji kura.

 

 

 

 

Share the love
September 6, 2023