Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB limetaka uchunguzi wa kina kufanywa kufuatia mauaji ya padre John Maina na Padre Alois Bett mtawalia.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, maaskofu wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Askofu mkuu Maurice Muhatia, wameeleza kuwa uchunguzi huo utafichua kiini cha mauaji hayo sawa na kuhakikisha kuwa usalama wa mapadre pamoja na wakenya unaimarishwa.
Aidha wamekashifu vikali mauaji yanayotekelezwa kufuatia mizozo ya kisiasa, wakisema kuwa wanaotekeleza mauaji hayo wamepoteza utu na umuhimu wa maisha ya binadamu.