Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB limeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini.

    Katika taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya taifa, maaskofu hao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Askofu mkuu Maurice Muhatia, wamerejelea mauaji ya wakenya ambayo yameshuhudiwa hivi karibuni yakiwemo ya mapadre wawili waliouwawa kwa njia tatanishi.

    Aidha wamesisitiza umuhimu wa maisha ya bindamu, wakisema kuwa kila mkenya ana haki ya kuishi bila uwoga wa kuuwawa.

    Kuhusu maandamano ya kesho, maaskofu hao wamewataka vijana kuandamana kwa njia ya Amani huku wakitoa changamoto kwa serikali kuwasilikiza vijana badala ya kuwakandamiza.

    June 24, 2025

    Leave a Comment