Kikosi cha wanajeshi wa KDF kinatarajiwa kuongoza shughuli za ujenzi wa uga wa Moi katika kaunti ya Embu, katika juhudi za kuharalkisha mchakato wa matayarisho kwa ajili ya sherehe za Maadhimisho ya siku ya Madaraka tarehe mosi mwezi Juni mwaka huu.

Makatibu wa wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu wa wizara ya mambo ya ndani Raymond Omollo, Pamoja na viongozi wa kaunti ya Embu akiwemo gavana Cicily Mbarire walizuru uga huo kutwa ya leo ili kukagua jinsi shughuli za ujenzi zinaendelea.

Maafisa hao wameeleza Imani yao kwamba shughuli za ujenzi huo zitakamilika mwezi mmoja kabla ya maadhimisho yenyewe kuandaliwa.

 

February 21, 2023