BY ISAYA BURUGU ,14TH NOV,2022-Aliyekuwa mwaniaji wa ugavana kaunti ya Narok kupitia tikiti ya ODM Moitalel Ole Kenta, mapema hii leo aliwasilisha ombi la kutaka kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa gavana wa sasa Patrick Ntutu.Mbunge huyo wa zamani wa Narok Kaskazini aliwasilisha ombi hilo mbele ya Jaji wa mahakama kuu ya Narok jaji Teresia Matheka.

Hatua ya Ole Kenta inafuatia juhudi za pamoja za watoa ushauri katika jamii ya Maa, miongoni mwao akiwa Askofu Mkuu wa ACK Jackson Ole Sapit, kusuluhisha mzozo huo nje ya mahakama.Ombi litasikilizwa mnamo Novemba 28, 2022.

Mnamo agosti, tume ya IEBC ilimtangaza Ntutu kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha ugavana wa Narok kwa kura 158,100 huku Ole Kenta akiibuka wa pili kwa kura 148,270.

Aidha Utangazaji wa matokeo rasmi ulicheleweshwa baada ya fujo kuzuka katika kituo cha kuhesabia kura cha kilgoris na kile cha Kaunti katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara, na kumlazimu msimamizi wa Uchaguzi Sidney Namulungu kutangaza matokeo kutoka Bomas Agosti 14.

November 14, 2022