BY ISAYA BURUGU ,14TH ,NOV,2022-Mwili wa mtoto wa miezi 9 umepatikana ukiwa umetupwa chooni katika mtaa wa total viungani mwa mji wa narok.Haya ni kwa mujibu wa mzee wa mtaa huo wa total jacob jomo ambaye amesema kwamba alipata taarifa hiyo kutoka kwa umma ambapo aliarifu maafisa wa polisi waliofika pale na kuuchukuwa mwili huo hadi hifadhi ya maiti kwenye hospitali ya rufaa ya narok.

Kadhalika, mzee jomo ameongeza pia mwili wa mtoto huyo ulikuwa umefunikwa na shuka na ulitolewa na wananchi kutoka kwa shimo hiyo kabla ya maafisa wa polisi kufika kwenye eneo la tukio.

Aidha mzee Jomo ametoa changamoto kwa wanawake ambao hawako tayari kupata watoto kujiepusha kufanya hivyo ili kuzuia visa vya kutupa watoto

 

November 14, 2022