Mataifa ya Kenya na Indonesia yatashirikiana katika sekta mbalimbali ili kuendelea kupiga jeki maendeleo na kukoleza mahusiano kati ya mataifa haya mawili. Haya yametangazwa na Rais William Ruto mapema leo katika Ikulu ya Nairobi, baada ya kumpokea Rais Joko Widodo wa Indonesia humu nchini mapema leo.

Rais huyo wa Indonesia ambaye ametua barani Afrika kwa mara ya kwanza, alipokelewa kwa heshima ya kijeshi katika ikulu ya Nairobi, huku viongozi hao wawili wa taifa wakiandaa vikao na kuafikia makubaliano hasa ya kibiashara.

Rais Joko Widodo ametembelea Kenya, akiwa ziarani kuelekea katika kikao cha mataifa yanakua kicuhumi cha BRICS kitakachoandaliwa hapo kesho nchini Afrika Kusini. Widodo atahudhuria mkutano huo huku kukiwa na minon’gono ya iwapo taifa lake huenda likajiunga na kundi hilo na kuwa mwanachama wake, lakini mwenyewe amesema serikali yake haijaamua kama itataka kujiunga na BRICS.

August 21, 2023