BY ISAYA BURUGU 21ST AUG 2023-Tamasha la siku nne la tamaduni za Jamii ya Maa zimeng’oa nanga katika Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara katika lango la Sekenani, Kaunti hii ya Narok.

Tamasha hilo linalonuia kusheherekea utamaduni wa jamii ya  maa kutoka Kote Kenya, limewaleta pamoja pia viongozi wa viwango mbalilmbali kutoka jamii ya maa, wakiwemo magavana wa kaunti za Narok, Kajiado na Samburu ambazo zinasheheni idadi kubwa ya wanajamii hawa.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria tamasha hilo ambalo litaendelea hadi siku ya Alhamisi ni pamoja na Waziri wa Utalii nchini Peninah Malonza, katibu mkuu katika idara ya Utalii Bw. John Ololtuaa, Katibu mkuu katika idara ya tamaduni Bi.

Ummi Bashir pamoja na katibu katika idara ya Wanyamapori Silvia Museiya.

 

 

 

 

 

Share the love
August 21, 2023