Aliyekuwa gavana wa kiambu Ferdinand Waititu amepata afueni baada ya mahakama kutupilia mbali kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Waititu alikuwa ameshtakiwa pamoja na wenzake 12 kwa kupanga njama ya kutoa zabuni ya barabara ya shilingi milioni 588 kwa kampuni za uwakilishi kinyume cha sheria.Miongoni mwa walioshtakiwa ni pamoja na mkewe Susan Wangari, aliyekuwa Afisa Mkuu wa barabra katika Kaunti ya Kiambu Luka Mwangi, wafanyikazi sita wa kaunti ya kiambu, mfanyabiashara Charles Chege na mkewe Beth Wangeci.

Waititu na mkewe wanadaiwa kupokea shilingi milioni 51 kutoka kwa kaunti kupitia kampuni zao Saika Two Estate Developers Ltd na Hoteli ya Benvenue Delta.Upande wa mashtaka umesema kuwa mpango wa kulaghai Serikali ya Kaunti ya Kiambu ulianzishwa na Chege na mkewe kupitia kampuni yao ya Testimony Enterprises mnamo Februari 26, 2018.

October 6, 2022