BY Isaya Burugu,Oct 7,2022– Maafisa wa polisi katika kaunti ya Siaya wanachunguza kisa ambapo maiti ilipatikana imezikwa kwenye boma la afisa wa ardhi Philip Onyango Ogutu miezi minne baada ya familia kuripoti kutoweka kwake.

Kwa mjibu wa naibu kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Alego Usonga Charles Odhiambo Kakaye Onyango aliripoti kuhusu kupatika kwa sehemu za mwili zilizopitaikana katika boma la  jamaa huyo.

Inaripotiwa kuwa jamaa mmoja aliyekuwa akikata nyasi kwenye boma hilo alipata mwili uliyokuwa umefunikwa kwa blanketi. Polisi wamelazimika kupata idhini ya kufukua mwili.

Jamaa huyo wa umri wa miaka 60 anasemekana kuwa amekuwa akiishi peke yake baada ya kutalakiana na mkewe.

 

October 7, 2022