By Isaya Burugu,Oct 7,2022-Maafisa wa polisi wamekuwa wakifanya oparesheni kurejesha mbuzi  walioibwa katika Kijiji cha Loikasi mjini  Maralal kaunti ya Samburu.

Hamsini kati ya mbuzi mia tatu na nane walioibwa mwezi jana wamepatikana.

Kwa Hisani

 

Wafugaji katika eneo hilo wanaitaka serikali kuimarisha usalama ili kuzuia visa vya wizi wa mifugo kwani unasababisha hasara kubwa.

Oparesheni hiyo inaongozwa na  naibu kamishna wa kaunti ya Samburu Titus Omanyi .

Polisi wanasema wanazidi kukifuatilia kisa hicho hadi waweze kurejesha mbuzi wote walioibwa

October 7, 2022