BY ISAYA BURUGU,13TH NOV,2023-Kiongozi wa Chama cha Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga ametoa changamoto kwa Rais William Ruto kutafuta njia mbadala za kupata mapato ya maendeleo nchini badala ya kuwatoza Wakenya ushuru mkubwa.

Odinga alimshutumu Rais Ruto kwa kuwakatisha tamaa Wakenya maskini na ushuru akisema ushuru sio suluhu ya kutatua mahitaji ya maendeleo ya Wakenya.Kiongozi huyo wa Upinzani alisema Wakenya tayari wamelemewa na gharama ya juu ya maisha ilhali utawala wa Kenya Kwanza umekuwa ukiendelea kuwatoza ushuru mara kwa mara.

Alisema familia nyingi haziwezi tena kukidhi mahitaji yao ya kila siku kutokana na ongezeko la ushuru wa bidhaa za kimsingi.Alimshutumu Ruto kwa kukosa jukumu lake la kupunguza gharama ya maisha kwa Wakenya.

Badala yake, alimtaka Ruto kufufua nafasi za kazi kama Kazi kwa Vijana na Kazi Mtaani ili kuimarisha mzunguko wa pesa nchini.

Odinga alikuwa akizungumza leo alipozindua harakati za usajili wa chama cha ODM ili kukabiliana na upenyezaji wa chama cha UDA katika ngome yake ya Nyanza.

 

 

 

 

November 13, 2023