BY ISAYA BURUGU 17TH FEB,2023-Kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga na viongozi wengine wamefika kaunti ya Kisii leo kwa ziara ya kukutana na wananchi. Odinga ameandamana na kinara wa wiper Kalonzo Musyoka, katibu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni ,kinara wa Nark Kenya Martha Karua,gavana  wa Kisii Simba Arati wabunge kati ya viongozi wengine.

Odinga na ujumbe wake wamezuru maeneo mbali mbali ya Kisii ikiwemo Keroka.Katika ziara hiyo viongozi waliozungumza wameikosoa serikali ya Kenya Kwanza kufuatia kile walichosema ni uongozi mbaya.

Kwa upande wake Odinga ameikosoa serikali   kwa kuendeleza mapendeleo katika uteuzi wa nyadhifa za umma huku kabila moja likinufaika .

Kilele cha mkutano wa leo kwa wana Azimio ni mkuano mkuu wa hadhara katika uwanja wa Kisii Kabla ya kuelekea Kisumu Kesho.

 

 

February 17, 2023