Rais William Ruto adhuhuri ya leo aliwasili mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kuhudhuria kongamano la 36 la marais wa muungano wa bara la Afrika.

Rais Ruto amejumuika na marais wa mataifa mbalimbali barani Afrika pamoja na viongozi wa serikali kuzungumzia mbinu za kuimarisha biashara kati ya mataifa yaliyoko bara Afrika.

Rais ametoa wito kwa uongozi wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuendesha utulivu nchini humo.

Kongamano hilo la siku tatu pia litatumika kushinikiza jumuiya ya kimataifa kuwajibika kuhusu ufadhili wa miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

February 17, 2023