Madaktari humu nchini wametishia kuanza mgomo iwapo mazungumzo kati yao na serikali kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja (CBA) wa 2017-2021 hayatazaa matunda.

Haya ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, Wanafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU) Dkt. Davji Bhimji Atellah, ambaye alizungumza baada ya Kongamano la Siku 2 la Wajumbe Maalum (SDC) lililofanyika katika kaunti ya Nakuru.

Dk Atellah, alisema makubaliano hayo yalisainiwa baada ya mgomo wa muda mrefu, lakini sasa inaonekana kupigwa na upepo, pamoja na malalamiko yao ambayo ni pamoja na nyongeza za mishahara na kuajiriwa kwa wafanyakazi.

Zaidi ya hayo, matabibu wamemshauri Rais William Ruto kuwaangazia matabibu katika serikali yake, hasa baada yao kufungiwa nje katika uteuzi wa kuhudumu kma makatibu wa kudumu, licha ya matatibu wapatao 250 kuwasilisha maombi yao.

November 26, 2022