Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) imetoa taarifa kuhusu hali ya Boniface Kariuki, mfanyabiashara aliyepigwa risasi wakati wa maandamano ya Jumanne jijini Nairobi.

    Akihutubia wanahabari Jumatano, Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa KNH Dkt. William Sigilai alisema kuwa Kariuki alipelekwa hospitalini humo baada kupewa rufaa kutoka hospitali moja iliyoko jiji la Nairobi.

    Ameeleza kuwa Timu ya wataalamu mbalimbali, walifanya upasuaji wa saa mbili ili kuondoa risasi iliyokuwa kichwani mwa Kariuki.

    Vilevile ameeleza kuwa walipokea jumla ya majeruhi 16 ambapo 9 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani huku 7 wakilazwa.

    June 18, 2025

    Leave a Comment