BY ISAYA BURUGU 19TH JULY 2023-Maaskofu wa kanisa katoliki nchini wamerejelea wito wao kwa rais Wiliam Ruto na kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga kufanya mazungumzo ili kusuluhisha utata ulioko nchini kwa sasa.

Wakizungumza na wandishi Habari mtaani Karen ,maaskofu hao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la maaskofu katoliki nchini KCCB Martin Kivuva wamesema kuwa viongozi hao wawili hawawezi endelea kusalia kimya huku nchi ikikaribia kutumbukia kwenye shida.

Wito wao unajiri huku mandamano yaliyopangwa na mungano wa Azimio la umoja yakirejelewa leo katika sehemu mbali mbali nchini.

Mandamano hayo ambayo yatakuwa yakiandaliwa kwa siku tatu kila wiki,yanashinikiza serikali kushughulikia gharama ya juu yakimaisha.

 

 

 

 

 

 

Share the love
July 19, 2023