Katibu mkuu wa  chama cha UDA Cleophas Malala amewataka viongozi wa upinzani kumpa rais Wiliam Ruto muda kutekeleza ahadi alizowapa wakenya wakati wa kampeni.

Akizungumza mjini Kakamega hivi leo,Malala amesema uongozi wa Kenya Kwanza umekuwa mammlakani kwa muda mfupi ambao hauwezi baini iwapo ahadi hizo zimetimizwa.

Kuhusu Mandamano ya mungano wa Azimio yanayoandaliwa leo kote nchini,Malala amesema ni haki ya kila mkenya kufanya mandamano lakini ni sharti yawe ya amani bila kuharibu mali ya wananchi.

Share the love
July 19, 2023