Siku moja baada ya Rais William Ruto kuwaonya viongozi wanaopinga mfumo wa ununuzi wa kidijitali E-procurement, wakuu wa kaunti wamekataa waziwazi msukumo wa kupitisha mfumo huo.

    Wakizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumatatu, magavana walijibu agizo hilo na msisitizo wa Waziri wa Hazina John Mbadi kwamba mashirika yote ya serikali lazima yanza kutumia mfumo huo wa kielektroniki.

    Wakuu hao wa kaunti walishutumu Hazina ya kitaifa kwa kuwatenga katika usambazaji wa mfumo wa ununuzi wa kidijitali na kutupilia mbali madai kwamba walikuwa wakizuia kimakusudi mageuzi.

    Walitaja dosari zinazoendelea katika Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Fedha (IFMIS), wakisema makosa yale yale huenda yakajirudia kwenye mfumo wa E-procurement.

    Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi, ambaye pia anahudumu kama mwenyekiti wa Baraza la Magavana, alimpinga  Mbadi, akisema kuwa serikali inaharakisha mchakato huo bila kushughulikia changamoto za kimsingi za kiufundi.

    Alionya dhidi ya vitisho , akisisitiza kwamba lazima mfumo huo mpya kwanza ufanyiwe majaribio na kurekebishwa vizuri kabla ya kuwekwa kwa kaunti zote.

    September 1, 2025

    Leave a Comment