BY ISAYA BURUGU,3RD MARCH,2023-Mahakama imebatiliza ushindi wa mbunge wa Legdera Abkadir Hussein Muhamed wa chama cha ODM aliyekuwa ameshinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana.

Hussein alikuwa amepata kura 5939 na kumshinda mpinzani wake wa UDA  Abdi Kani Zeituni aliyepata kura 4863. Hiyo ni maana kuwa uchaguzi utandaliwa tena katika eneo bunge hilo. Muhamed amepa kukata rufaa uamuzi huo wa mahakama.

Wakati huo huo mahakama kuu imepuzilia mbali  kesi iliyokuwa ikipinga ushindi wa gavana  wawajir Ahmed Abdullahi katika uchaguzi mkuu uliyopita.Jaji George Dulu ameshikilia ushindi wa  Abdullahi’ na kutupilia mbali kesi iliyowasilsihwa dhidi ya ushindi huo na Adan Mohamed Hassan wa Jubilee aliyepoteza.Jaj huyo akiketi katika mahakama ya Milimani Nairobi amesema mlalamishi alikosa kudhibitisha kuwa Abdullahi, aliyeshinda kwa tiketi ya chama chaa ODM hakushinda kihalali.

Tusalie mahakamani ambapo mahakama kuu huko Malindi imefitilia mbali ushindi wa  Harrison Garama Kombe  wa  ODM kama mbunge wa eneo bunge la Magarini kufuatia visa vingi vya ukukaji sheria.

Mgombea wachama cha  UDA Stanley Kenga alikuwa amewasilisha kesi kupinga ushindi wa Kombe katika uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

March 3, 2023